Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 15:1-16 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 15:1-16 in Biblia ya Kiswahili

1 Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.
2 Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.
3 Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.
4 Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.
5 Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.
6 Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata JIwe la Bohani mwana wa Rubeni.
7 Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za Eni Shemeshi na kufika Eni Rogeli.
8 kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi (ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kasikazini.
9 Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala (ambao ndio Kiriathi Yearimu).
10 Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.
11 Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kasikazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambasamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.
12 Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.
13 Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
14 Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.
15 Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
16 Kalebu akasema, “Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.
Yoshua 15 in Biblia ya Kiswahili