Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 15

Yoshua 15:1-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.
2Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.
3Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.
4Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.
5Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.
6Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata JIwe la Bohani mwana wa Rubeni.
7Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za Eni Shemeshi na kufika Eni Rogeli.
8kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi (ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kasikazini.
9Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala (ambao ndio Kiriathi Yearimu).
10Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.
11Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kasikazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambasamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.
12Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.
13Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
14Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.
15Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
16Kalebu akasema, “Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.

Read Yoshua 15Yoshua 15
Compare Yoshua 15:1-16Yoshua 15:1-16