Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 7:1-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 7:1-9 in Biblia Takatifu

1 Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya. Hakutaka kutembea mkoani Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wanataka kumwua.
2 Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
3 Basi ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.
4 Mtu hafanyi mambo kwa siri kama anataka kujulikana kwa watu. Maadam unafanya mambo haya, basi, jidhihirishe kwa ulimwengu.”
5 (Hata ndugu zake hawakumwamini!)
6 Basi, Yesu akawaambia, “Wakati wangu ufaao haujafika bado. Lakini kwenu ninyi kila wakati unafaa.
7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nauambia wazi kwamba matendo yake ni maovu.
8 Ninyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika.”
9 Alisema hayo kisha akabaki huko Galilaya.
Yohana 7 in Biblia Takatifu

Yohana 7:1-9 in Biblia ya Kiswahili

1 Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
2 Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
3 Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
4 Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”
5 Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
6 Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
8 Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.”
9 Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
Yohana 7 in Biblia ya Kiswahili