Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 7

Yohana 7:1-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
2Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
3Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
4Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”
5Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
6Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
7Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
8Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.”
9Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.

Read Yohana 7Yohana 7
Compare Yohana 7:1-9Yohana 7:1-9