Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 5:34-43 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 5:34-43 in Biblia Takatifu

34 Si kwamba mimi nautegemea ushahidi wa wanadamu, lakini nasema mambo haya ili mpate kuokolewa.
35 Yohane alikuwa kama taa iliyokuwa ikiwaka na kuangaza, nanyi mlikuwa tayari kufurahia mwanga huo kwa kitambo.
36 Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.
37 Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,
38 na ujumbe wake haukai ndani yenu maana hamkumwamini yule aliyemtuma.
39 Ninyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uzima wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!
40 Hata hivyo, ninyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima.
41 “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu.
42 Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
43 Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea.
Yohana 5 in Biblia Takatifu

Yohana 5:34-43 in Biblia ya Kiswahili

34 Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
35 Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.
36 Ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.
37 Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.
38 Hamna neno lake likikaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.
39 Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na
40 hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.
41 Sipokei sifa kutoka kwa watu,
42 lakini ninajua kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu ninyi wenyewe.
43 Nimekuja kwa jina la Baba yangu, hamukuweza kunipokea. Kama mwingine akija kwa jina lake mngempokea.
Yohana 5 in Biblia ya Kiswahili