Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 5

Yohana 5:34-43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
34Si kwamba mimi nautegemea ushahidi wa wanadamu, lakini nasema mambo haya ili mpate kuokolewa.
35Yohane alikuwa kama taa iliyokuwa ikiwaka na kuangaza, nanyi mlikuwa tayari kufurahia mwanga huo kwa kitambo.
36Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.
37Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,
38na ujumbe wake haukai ndani yenu maana hamkumwamini yule aliyemtuma.
39Ninyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uzima wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!
40Hata hivyo, ninyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima.
41“Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu.
42Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
43Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea.

Read Yohana 5Yohana 5
Compare Yohana 5:34-43Yohana 5:34-43