Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 4:2-10 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 4:2-10 in Biblia Takatifu

2 (Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.)
3 Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;
4 na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.
5 Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
6 Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
7 Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, “Nipatie maji ninywe.”
8 (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)
9 Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu.)
10 Yesu akamjibu, “Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekwambia: Nipatie maji ninywe, ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai.”
Yohana 4 in Biblia Takatifu

Yohana 4:2-10 in Biblia ya Kiswahili

2 (ingawa Yesu mwenyewe alikuwa habatizi ila wanafunzi wake),
3 alitoka Judea na akaenda Galilaya.
4 Hivyo ilikuwa muhimu kupitia Samaria.
5 Na akafika kwenye mji wa Samaria, unaoitwa Sikari, karibu na eneo ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu.
6 Na kisima cha Yakobo kilikuwa hapo. Yesu alikuwa amechoka kwa ajili ya safari na akakaa karibu na kisima. Ilikuwa muda wa mchana.
7 Mwanamke Msamaria alikuja kuteka maji, na Yesu akamwambia, “Nipe maji ninywe.”
8 Kwa sababu wanafunzi wake walikuwa wameenda zao mjini kununua chakula.
9 Yule mwanamke akamwambia, “Inakuaje wewe Myahudi, kuniomba mimi mwanamke Msamaria, kitu cha kunywa?” Kwa sababu Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.
10 Yesu akamjibu, “Kama ungelijua karama ya Mungu, na yule anayekuambia 'Nipe maji,' ungelimwomba, na angelikupa maji ya uzima.”
Yohana 4 in Biblia ya Kiswahili