Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 3:1-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 3:1-9 in Biblia Takatifu

1 Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo.
2 Siku moja alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.”
3 Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona ufalme wa Mungu.”
4 Nikodemo akamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa mara ya pili!”
5 Yesu akamjibu, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.
6 Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho.
7 Usistaajabu kwamba nimekwambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya.
8 Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
9 Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”
Yohana 3 in Biblia Takatifu

Yohana 3:1-9 in Biblia ya Kiswahili

1 Basi kulikuwa na Farisayo ambaye jina lake Nikodemo, mmoja wa wajumbe wa baraza la Wayahudi.
2 Mtu huyu alimwendea Bwana Yesu usiku na akamwambia, “Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu kutoka kwa Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kutenda ishara hizi zote Mungu asipokuwa pamoja naye.”
3 Yesu akamjibu, “Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.”
4 Nikodemo akasema,” Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, je anaweza?”
5 Yesu akajibu, “Amini, amini mtu sipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usishangae kwa sababu nilikuwambia, 'ni lazima kuzaliwa mara ya pili.'
8 Upepo huvuma popote upendapo na sauti yake mwaisikia, lakini hamjui utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo hali ya kila aliyezaliwa na roho.
9 Nikodemo akajibu, kwa kusema, “Mambo haya yawezekanaje?”
Yohana 3 in Biblia ya Kiswahili