29Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!
30huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, “Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.'
31Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, kwamba nilikuja nikibatiza kwa maji.”
32Yohana alishuhudia, “Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa hua, na ilibaki juu yake.
33Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, 'yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, Huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.'
34Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu.”