Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 1

Yohana 1:2-41

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu.
3Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika.
4Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote.
5Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuizimisha.
6Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye jina lake alikuwa Yohana.
7Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye.
8Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru
9Hiyo ilikuwa nuru ya kweli ambayo ilikuwa inakuja katika dunia nayo humtia nuru kila mmoja
10Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, na dunia haikumjua.
11Alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea.
12Bali kwa wale wengi waliompokea, ambao waliamini jina lake, kwa hao aliwapa haki ya kuwa wana wa Mungu,
13Ambao walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe.
14Naye Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu, tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa mtu pekee wa kipekee aliyekuja kutoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.
15Yohana alishuhudia kuhusu yeye, na alipaza sauti akisema, “Huyu ndiye ambaye nilisema habari zake nikisema, “Yule ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu amekuwako kabla yangu.”
16Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea bure kipawa baada ya kipawa.
17Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo.
18Hakuna mwanadamu aliyemwona Mungu wakati wowote. Mtu pekee ambaye ni Mungu, aliye katika kifua cha Baba, amemfanya yeye ajulikane.
19Na huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati makuhani na walawi waliotumwa kwake na Wayahudi kumwuliza, “Wewe ni nani?”
20Bila kusitasita na hakukana, bali alijibu, “Mimi sio Kristo.”
21Hivyo wakamuuliza, “kwa hiyo wewe ni nani sasa?” Wewe ni Eliya? Akasema, “Mimi siye.” Wakasema, Wewe ni nabii? Akajibu,” Hapana.”
22Kisha wakamwambia, “Wewe ni nani, ili kwamba tuwape jibu waliotutuma”? Wajishuhudiaje wewe mwenyewe?”
23Akasema, “Mimi ni sauti yake aliaye nyikani: 'Inyosheni njia ya Bwana,' kama nabii Isaya alivyosema.”
24Basi kulikuwa na watu wametumwa pale kutoka kwa Mafarisayo. Wakamuuliza na kusema,
25“Kwa nini unabatiza basi kama wewe sio Kristo wala Eliya wala nabii?”
26Yohana aliwajibu akisema, “Ninabatiza kwa maji. Hata hivyo, miongoni mwenu anasimama mtu msiyemtambua.
27Huyu ndiye ajaye baada yangu. Mimi sisitahili kulegeza kamba za viatu vyake.”
28Mambo haya yalitendeka huko Bethania, ng'ambo ya Yordani, mahali ambapo Yohana alikuwa akibatiza.
29Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!
30huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, “Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.'
31Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, kwamba nilikuja nikibatiza kwa maji.”
32Yohana alishuhudia, “Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa hua, na ilibaki juu yake.
33Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, 'yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, Huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.'
34Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu.”
35Tena siku iliyofuata Yohana alikuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili,
36walimwona Yesu akitembea na Yohana akasema, “Tazama, Mwana kondoo wa Mungu!”
37Wanafunzi wawili walimsikia Yohana akisema haya wakamfuata Yesu.
38Tena Yesu aligeuka na kuwaona wanafunzi wale wakimfuata, na akawambia, “Mnataka nini?” Wakajibu, “Rabbi, (maana yake 'mwalimu,' unaishi wapi?”
39Akawambia, “Njooni na mwone.” Kisha walikwenda na kuona mahali alipokuwa akiishi; walikaa pamoja naye siku hiyo, kwa kuwa ilikuwa yapata kama saa kumi hivi.
40Mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro.
41Akamwona ndugu yake Simoni na akamwambia, “Tumempata Masihi” (ambayo inatafsiriwa Kristo).

Read Yohana 1Yohana 1
Compare Yohana 1:2-41Yohana 1:2-41