7Niambie, wewe ninaye kupenda, wapi unalisha mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
8Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
9Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.