Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Warumi 12:1-13 in Swahili (individual language)

Help us?

Warumi 12:1-13 in Biblia Takatifu

1 Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
2 Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
3 Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
4 Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
5 Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
8 Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
9 Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
10 Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima.
11 Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
12 Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima.
13 Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.
Warumi 12 in Biblia Takatifu

Warumi 12:1-13 in Biblia ya Kiswahili

1 Kwa hiyo nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, inayokubalika kwa Mungu. Hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu.
3 Kwa maana nasema, kwa sababu ya neema niliyopewa, kwamba kila mtu ambaye yupo miongoni mwenu hapaswi kufikiri zaidi juu yake mwenyewe kuliko inavyompasa kufikiri. Bali, imempasa kufikiri kwa hekima, kama ambavyo Mungu amewapa kila mmoja kiasi fulani cha imani.
4 Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja.
5 Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.
6 Tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadiri ya neema mliyopewa. Ikiwa karama ya mtu ni unabii, na itendeke kwa kadiri ya imani yake.
7 Ikiwa karama ya mtu ni huduma, na atumike. Ikiwa mwingine ana karama ya kufundisha, basi, afundishe.
8 Ikiwa karama ya mtu ni faraja, basi, afariji. Ikiwa karama ya mtu ni kutoa, afanye hivyo kwa ukarimu. Ikiwa karama ya mtu ni kuongoza, na litendeke kwa uangalifu. Ikiwa karama ya mtu ni katika kuonesha huruma, na litendeke kwa furaha.
9 Pendo lisiwe na unafiki. Chukieni uovu; mshikilie yaliyo mema.
10 Kuhusu upendo wa ndugu, pendaneni ninyi kwa ninyi. Kuhusu heshima, heshimianeni ninyi kwa ninyi.
11 Kuhusu bidii, msiwe walegevu. Kuhusu roho, iweni na shauku. Kuhusu Bwana, mtumikieni.
12 Furahini katika ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo. Muwe na subira katika matatizo yenu. Mdumu katika kuomba.
13 Mshiriki katika mahitaji ya waumini. Tafuteni njia nyingi za kuonesha ukarimu.
Warumi 12 in Biblia ya Kiswahili