Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Warumi - Warumi 12

Warumi 12:1-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
2Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
3Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
4Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
5Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
6Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
7Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
8Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
9Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
10Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima.
11Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
12Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima.
13Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.

Read Warumi 12Warumi 12
Compare Warumi 12:1-13Warumi 12:1-13