Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Warumi 11:7-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Warumi 11:7-9 in Biblia Takatifu

7 Sasa, je? Watu wa Israeli hawakukipata kile walichokuwa wanakitafuta; lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine walipumbazwa,
8 kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mungu ameifanya mioyo yao kuwa mizito, na mpaka leo hii hawawezi kuona kwa macho yao wala kusikia kwa masikio yao.”
9 Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa, waanguke na kuadhibiwa.
Warumi 11 in Biblia Takatifu

Warumi 11:7-9 in Biblia ya Kiswahili

7 Ni nini basi? Jambo ambalo Israeli alikuwa akitafuta, hakukipata, bali wateule walikipata, na wengine walitiwa uzito.
8 Ni kama ilivyoandikwa: “Mungu amewapa roho ya ubutu, macho ili wasione, na masikio ili wasisikie, mpaka leo hii.”
9 Naye Daudi anasema, “Acha meza zao na ziwe wavu, mtego, sehemu ya kujikwaa, na kulipiza kisasi dhidi yao.
Warumi 11 in Biblia ya Kiswahili