Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 6:4-25 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 6:4-25 in Biblia ya Kiswahili

4 Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia.
5 Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege.
6 Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara.
7 Hana akida, afisa au mtawala,
8 lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
9 Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?”
10 Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo” -
11 ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita.
12 Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake,
13 akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.
14 Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.
15 Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.
16 Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.
17 Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,
18 moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,
19 shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.
20 Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21 Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.
22 utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.
23 Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima.
24 Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi.
25 Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake.
Mithali 6 in Biblia ya Kiswahili