Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 6

Mithali 6:4-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia.
5Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege.
6Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara.
7Hana akida, afisa au mtawala,
8lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
9Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?”
10Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo” -
11ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita.
12Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake,
13akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.
14Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.
15Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.
16Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.
17Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,
18moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,
19shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.
20Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.
22utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.
23Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima.
24Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi.
25Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake.

Read Mithali 6Mithali 6
Compare Mithali 6:4-25Mithali 6:4-25