Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 15:25-31 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 15:25-31 in Biblia ya Kiswahili

25 Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
26 Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
27 Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
28 Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.
29 Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki.
30 Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili.
31 Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara.
Mithali 15 in Biblia ya Kiswahili