Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 3

Mhubiri 3:7-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7wakati kuchana mavazi na wakati wa kuyashona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza.
8Kuna wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.
9Ni faida gani mfanyakazi aipatayo katika kazi yake?
10Nimeona kazi ambayo Mungu amewapa wanadamu kuitimiza.
11Mungu amefanya kila kitu kufaa kwa wakati wake. Pia ameweka umilele ndani ya mioyo yao. Lakini mwanadamu hawezi kuelewa matendo ambayo Mungu ameyafanya, tangu mwanzo wao hadi mwisho.
12Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi-
13na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
14Ninajua kwamba chochote afanyacho Mungu kinadumu milele. Hakuna kinaweza kuongezwa au kuondolea, kwa sababu Mungu ndiye aliyekifanya, ili kwamba watu wamsogelee kwa heshima.
15Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo; chochote kitakachokuwepo kimekwisha kuwepo. Mungu huwafanya wanadamu kutafuka vitu vilivyjificha.
16Na nimeona kwamba chini ya jua ubaya upo mahali palipopaswa kuwa na haki, na sehemu ya haki mara nyingi ina ubaya.

Read Mhubiri 3Mhubiri 3
Compare Mhubiri 3:7-16Mhubiri 3:7-16