Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 9:2-25 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 9:2-25 in Biblia Takatifu

2 akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia ya Bwana, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
3 Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga kutoka angani ulimwangazia pande zote.
4 Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: “Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?”
5 Naye Saulo akauliza, “Ni nani wewe Bwana?” Na ile sauti ikajibu, “Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa.
6 Lakini simama sasa, uingie mjini na huko utaambiwa unachopaswa kufanya.”
7 Wale watu waliokuwa wanasafiri pamoja na Saulo walisimama pale, wakiwa hawana la kusema; walisikia ile sauti lakini hawakumwona mtu.
8 Saulo aliinuka, na alipofumbua macho yake hakuweza kuona chochote; hivyo wale watu wakamwongoza kwa kumshika mkono mpaka mjini Damasko.
9 Saulo alikaa siku tatu bila kuona, na wakati huo hakula au kunywa chochote.
10 Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, “Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa, Bwana.”
11 Naye Bwana akamwambia, “Jitayarishe uende kwenye barabara inayoitwa Barabara ya Moja kwa Moja, na katika nyumba ya Yuda umtake mtu mmoja kutoka Tarso aitwaye Saulo. Sasa anasali;
12 na katika maono ameona mtu aitwaye Anania akiingia ndani na kumwekea mikono ili apate kuona tena.”
13 Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kutoka kwa watu wengi; nimesikia juu ya mabaya aliyowatendea watu wako huko Yerusalemu.
14 Na amekuja hapa akiwa na mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu kuwatia nguvuni wote wanaoomba kwa jina lako.”
15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli.
16 Mimi mwenyewe nitamwonyesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu.”
17 Basi, Anania akaenda, akaingia katika hiyo nyumba. Kisha akaweka mikono yake juu ya Saulo, akasema, “Ndugu Saulo, Bwana ambaye ndiye Yesu mwenyewe aliyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa, amenituma ili upate kuona tena na kujazwa Roho Mtakatifu.”
18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka macho ya Saulo, akaweza kuona tena. Akasimama, akabatizwa.
19 Na baada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia. Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasi huko Damasko.
20 Mara alianza kuhubiri katika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
21 Watu wote waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, mtu huyu si yuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaomba kwa jina hili kule Yerusalemu? Tena alikuja hapa akiwa na madhumuni ya kuwatia nguvuni watu hao na kuwapeleka kwa makuhani!”
22 Saulo alizidi kupata nguvu, na kwa jinsi alivyothibitisha wazi kwamba Yesu ndiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko walivurugika kabisa.
23 Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi walikusanyika na kufanya mpango wa kumwua Saulo.
24 Lakini Saulo alipata habari ya mpango huo. Usiku na mchana walilinda milango ya kuingia mjini ili wapate kumwua.
25 Lakini wakati wa usiku wanafunzi wake walimchukua, wakamteremsha chini ndani ya kapu kubwa kwa kupitia nafasi iliyokuwako ukutani.
Matendo 9 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 9:2-25 in Biblia ya Kiswahili

2 na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3 Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,'
4 naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?”
5 Sauli akajibu, U nani wewe Bwana? Bwana akasema, “Mimi ndiye Yesu unayeniudhi;
6 Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda
7 Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakatulia kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu.
8 Sauli akainuka katika nchi na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9 Kwa siku tatu haoni, hali, wala hanywi.
10 Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania, Bwana alisema naye katika maono, “Anania.” Na akasema, “Tazama, nipo hapa, Bwana.
11 “Bwana akamwambia, “Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba;
12 na alimwona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili kwamba apate kuona.
13 Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, kwa kiasi gani alivyowatendea mabaya watakatifu wa huko Yerusalemu;
14 Hapa ana mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kumkamata kila mmoja anayeliitia jina lako.
15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, alichukue jina langu mbele ya Mataifa na wafalme na wana wa Israeli.
16 Maana nitawaonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu”.
17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani; Akamwekea mikono akasema, Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.
18 Ghafla vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula na kupata nguvu.
19 Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi.
20 Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
21 Na wote waliosikia walishangaa na kusema, “Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani.”
22 Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri na kuwafanya Wayahudi waliokaa Dameski wachanganyikiwe na kuthibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
23 Baada ya siku nyingi, Wayahudi wakafanya shauri pamoja ili wamuue.
24 Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua.
25 Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu.
Matendo ya Mitume 9 in Biblia ya Kiswahili