Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 9

Matendo ya Mitume 9:2-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,'
4naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?”
5Sauli akajibu, U nani wewe Bwana? Bwana akasema, “Mimi ndiye Yesu unayeniudhi;
6Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda
7Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakatulia kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu.
8Sauli akainuka katika nchi na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9Kwa siku tatu haoni, hali, wala hanywi.
10Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania, Bwana alisema naye katika maono, “Anania.” Na akasema, “Tazama, nipo hapa, Bwana.
11“Bwana akamwambia, “Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba;
12na alimwona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili kwamba apate kuona.
13Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, kwa kiasi gani alivyowatendea mabaya watakatifu wa huko Yerusalemu;
14Hapa ana mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kumkamata kila mmoja anayeliitia jina lako.
15Lakini Bwana akamwambia, “Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, alichukue jina langu mbele ya Mataifa na wafalme na wana wa Israeli.
16Maana nitawaonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu”.
17Anania akaenda, akaingia mle nyumbani; Akamwekea mikono akasema, Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.
18Ghafla vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula na kupata nguvu.
19Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi.
20Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
21Na wote waliosikia walishangaa na kusema, “Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani.”
22Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri na kuwafanya Wayahudi waliokaa Dameski wachanganyikiwe na kuthibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
23Baada ya siku nyingi, Wayahudi wakafanya shauri pamoja ili wamuue.
24Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua.
25Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu.

Read Matendo ya Mitume 9Matendo ya Mitume 9
Compare Matendo ya Mitume 9:2-25Matendo ya Mitume 9:2-25