Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 8:4-11 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 8:4-11 in Biblia Takatifu

4 Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe.
5 Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwa wenyeji wa hapo.
6 Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
7 Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi waliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo na waliolemaa waliponywa.
8 Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.
9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
10 Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini wakisema, “Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa Nguvu Kubwa.”
11 Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake kwa muda mrefu.
Matendo 8 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 8:4-11 in Biblia ya Kiswahili

4 waaminio ambao walikuwa wametawanyika bado walilihubiri neno.
5 Filipo akashuka katika mji wa Samaria na akamtangaza Kristo huko.
6 Baada ya makutano kusikia na kuona ishara alizofanya Filipo; wakaweka umakini juu ya kile alichosema.
7 Kutoka hapo watu wengi waliosikia, pepo wachafu waliwatoka watu huku wakilia kwa sauti kubwa, na wengi waliopooza na viwete waliponywa.
8 Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji.
9 Lakini palikuwa na mtu mmoja katika mji ule jina lake Simon, ambaye alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu.
10 Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa, wakamsikiliza; wakasema;” mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu.”
11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mrefu kwa uchawi wake.
Matendo ya Mitume 8 in Biblia ya Kiswahili