Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 2:44-47 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 2:44-47 in Biblia Takatifu

44 Waumini wote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zao waligawana pamoja.
45 Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja.
46 Waliendelea kukutana pamoja kila siku Hekaluni. Lakini wakati wa kumega mkate, walikutana katika nyumba zao na wakakishiriki chakula hicho kwa furaha na moyo mkunjufu.
47 Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
Matendo 2 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 2:44-47 in Biblia ya Kiswahili

44 Wote walioamini walikuwa pamoja na kuwa na vitu vyao kwa pamoja,
45 na waliuza vitu na milki zao na kugawanya kwa wote kulingana na hitaji la kila mmoja.
46 Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu, na walimega mkate kwenye kaya, na walishiriki chakula kwa furaha na unyenyekevu wa moyo;
47 walimsifu Mungu na wakiwa na kibali na watu wote. Bwana aliwaongeza siku kwa siku ambao walikuwa wakiokolewa.
Matendo ya Mitume 2 in Biblia ya Kiswahili