2 Petro alipokuja huko Yerusalemu, lile kundi la watu waliotahiriwa wakaanza kumkosoa, Wakisema,
3 “Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!”
4 Lakini Petro alianza kueleza tukio kwa kina; akisema,
5 “Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu.
6 Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa polini na wanyama watambaao na ndege wa angani.
7 Kisha nikasikia sauti ikisema nami, “Amka, Petro, chinja naj ule!”
8 Nikasema, “Siyo hivyo, Bwana, mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu”
9 Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi,
10 Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.