Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 11:18-30 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 11:18-30 in Biblia Takatifu

18 Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu na kuwa na uzima!”
19 Kutokana na mateso yaliyotokea wakati Stefano alipouawa, waumini walitawanyika. Wengine walikwenda mpaka Foinike, Kupro na Antiokia wakihubiri ule ujumbe kwa Wayahudi tu.
20 Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria ile Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
21 Bwana aliwasaidia na idadi kubwa ya watu iliamini na kumgeukia Bwana.
22 Habari ya jambo hilo ikasikika kwa lile kanisa la Yerusalemu. Hivyo wakamtuma Barnaba aende Antiokia.
23 Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
24 Barnaba alikuwa mtu mwema na mwenye kujaa Roho Mtakatifu na imani. Kundi kubwa la watu lilivutwa kwa Bwana.
25 Kisha, Barnaba alikwenda Tarso kumtafuta Saulo
26 Alipompata, alimleta Antiokia. Nao wote wawili walikaa na lile kanisa kwa mwaka wote mzima wakifundisha kundi kubwa la watu. Huko Antiokia, ndiko, kwa mara ya kwanza, wafuasi waliitwa Wakristo.
27 Wakati huohuo, manabii kadhaa walikuja Antiokia kutoka Yerusalemu.
28 Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote (Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa akitawala).
29 Wale wanafunzi waliamua kila mmoja kwa kadiri ya uwezo wake apeleke chochote ili kuwasaidia wale ndugu waliokuwa wanaishi Yudea.
30 Basi, wakafanya hivyo na kupeleka mchango wao kwa wazee wa kanisa kwa mikono ya Barnaba na Saulo.
Matendo 11 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 11:18-30 in Biblia ya Kiswahili

18 Waliposikia mambo haya, hawakurudisha, bali walimsifu Mungu na kusema, “Mungu ametoa toba kwa ajili ya wa mataifa pia”
19 Basi waamini ambao mateso yalianzia kwenye kifo cha Stephano walitawanyika kutoka Yerusalemu-waamini hawa walienda mbali, hadi mpaka Foinike, Kipro na Antiokia. Waliwaambia ujumbe kuhusu Yesu peke yake kwa wayahudi na si kwa mwingine awaye yote.
20 Lakini baadhi yao ni watu kutoka Kipro na Krene, walikuja Antiokia na kusema na wayunani na kumhubiri Bwana Yesu.
21 Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, na watu wengi waliamini na kumgeukia Bwana.
22 Habari zao zikafikia masikioni mwa kanisa la Yerusalem: na wakamtuma Barnaba aende mpaka Antiokia.
23 Alipokuja na kuona karama ya Mungu alifurahi; na aliwatia moyo wote kubaki na Bwana katika mioyo yao.
24 Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka katika Bwana.
25 Baadaye Barnaba alienda Tarso kumwona Sauli.
26 Alipompata, akamleta Antiokia. Ikawa kwa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi wakaitwa wakristo kwa mara ya kwanza huko Antiokia.
27 Na katika siku hizi manabii wakashuka kutoka Yerusalemu mpaka Antiokia.
28 Mmoja wao ni Agabo ndilo jina lake, akasimama akiashiriwa na Roho kuwa njaa kali itatokea ulimwenguni mwote. Hii ilitokea wakati wa siku za Klaudio.
29 Kwa hiyo, wanafunzi, kila mmoja alivyo fanikiwa, waliamua kupeleka misaada kwa ndugu walioko Uyahudi.
30 Walifanya hivi; Walituma pesa kwa mkono wa Barnaba na Sauli.
Matendo ya Mitume 11 in Biblia ya Kiswahili