Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 11:10-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 11:10-19 in Biblia Takatifu

10 Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni.
11 Ghafla, watu watatu waliokuwa wametumwa kwangu kutoka Kaisarea waliwasili kwenye nyumba niliyokuwa nakaa.
12 Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa Kornelio.
13 Yeye alitueleza jinsi alivyokuwa amemwona malaika amesimama nyumbani mwake na kumwambia: Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.
14 Yeye atakuambia maneno ambayo kwayo wewe na jamaa yako yote mtaokolewa.
15 Na nilipoanza tu kuongea, Roho Mtakatifu aliwashukia kama alivyotushukia sisi pale awali.
16 Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: Yohane alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.
17 Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine zawadi ileile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani hata nijaribu kumpinga Mungu?”
18 Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu na kuwa na uzima!”
19 Kutokana na mateso yaliyotokea wakati Stefano alipouawa, waumini walitawanyika. Wengine walikwenda mpaka Foinike, Kupro na Antiokia wakihubiri ule ujumbe kwa Wayahudi tu.
Matendo 11 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 11:10-19 in Biblia ya Kiswahili

10 Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.
11 Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu.
12 Roho akaniambia kwenda nao, na nisitofautiane nao. Hawa wanaume sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu mmoja.
13 Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, “Nitume Yafa nikamlete simoni ambaye jina lake lingine ni Petro.
14 Atasema ujumbe kwako katika huo utaokoka wewe na nyumba yako yote.”
15 Nilipoanza kusema nao, Roho mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni.
16 Nakumbuka maneno ya Bwana, alivyosema, “Yohana alibatiza kwa maji; lakini mtabatizwa katika Roho mtakatifu.”
17 Pia kama Mungu ametoa zawadi kama alizotupa sisi tulipoamini katika Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani, kwamba naweza kumpinga Mungu?
18 Waliposikia mambo haya, hawakurudisha, bali walimsifu Mungu na kusema, “Mungu ametoa toba kwa ajili ya wa mataifa pia”
19 Basi waamini ambao mateso yalianzia kwenye kifo cha Stephano walitawanyika kutoka Yerusalemu-waamini hawa walienda mbali, hadi mpaka Foinike, Kipro na Antiokia. Waliwaambia ujumbe kuhusu Yesu peke yake kwa wayahudi na si kwa mwingine awaye yote.
Matendo ya Mitume 11 in Biblia ya Kiswahili