Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 9:17-39 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 9:17-39 in Biblia Takatifu

17 Basi, Anania akaenda, akaingia katika hiyo nyumba. Kisha akaweka mikono yake juu ya Saulo, akasema, “Ndugu Saulo, Bwana ambaye ndiye Yesu mwenyewe aliyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa, amenituma ili upate kuona tena na kujazwa Roho Mtakatifu.”
18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka macho ya Saulo, akaweza kuona tena. Akasimama, akabatizwa.
19 Na baada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia. Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasi huko Damasko.
20 Mara alianza kuhubiri katika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
21 Watu wote waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, mtu huyu si yuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaomba kwa jina hili kule Yerusalemu? Tena alikuja hapa akiwa na madhumuni ya kuwatia nguvuni watu hao na kuwapeleka kwa makuhani!”
22 Saulo alizidi kupata nguvu, na kwa jinsi alivyothibitisha wazi kwamba Yesu ndiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko walivurugika kabisa.
23 Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi walikusanyika na kufanya mpango wa kumwua Saulo.
24 Lakini Saulo alipata habari ya mpango huo. Usiku na mchana walilinda milango ya kuingia mjini ili wapate kumwua.
25 Lakini wakati wa usiku wanafunzi wake walimchukua, wakamteremsha chini ndani ya kapu kubwa kwa kupitia nafasi iliyokuwako ukutani.
26 Saulo alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na wale wanafunzi. Lakini wote walimwogopa, na hawakuweza kuamini kwamba yeye amekuwa mfuasi.
27 Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila uoga kule Damasko.
28 Basi, Saulo alikaa pamoja nao, akatembelea Yerusalemu yote akihubiri neno la Bwana bila hofu.
29 Pia aliongea na kubishana na Wayahudi wasemao Kigiriki, lakini wao walijaribu kumwua.
30 Wale ndugu walipogundua jambo hilo walimchukua Saulo, wakampeleka Kaisarea, wakamwacha aende zake Tarso.
31 Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.
32 Petro alipokuwa anasafirisafiri kila mahali alifika pia kwa watu wa Mungu waliokuwa wanaishi Luda.
33 Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Enea ambaye kwa muda wa miaka minane alikuwa amelala kitandani kwa sababu alikuwa amepooza.
34 Basi, Petro akamwambia, “Enea, Yesu Kristo anakuponya. Amka utandike kitanda chako.” Enea akaamka mara.
35 Wakazi wote wa Luda na Saroni walimwona Enea, na wote wakamgeukia Bwana.
36 Kulikuwa na mfuasi mmoja mwanamke mjini Yopa aitwaye Tabitha (kwa Kigiriki ni Dorka, maana yake, Paa). Huyo mwanamke alikuwa akitenda mema na kuwasaidia maskini daima.
37 Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakauzika katika chumba ghorofani.
38 Yopa si mbali sana na Luda; kwa hiyo wafuasi waliposikia kwamba Petro alikuwa Luda, wakawatuma watu wawili kwake na ujumbe: “Njoo kwetu haraka iwezekanavyo.”
39 Basi, Petro akaenda pamoja nao. Alipofika alipelekwa ghorofani katika kile chumba. Huko wajane wengi walimzunguka Petro wakilia na kumwonyesha makoti na nguo ambazo Dorka alikuwa akitengeneza wakati alipokuwa hai.
Matendo 9 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 9:17-39 in Biblia ya Kiswahili

17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani; Akamwekea mikono akasema, Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.
18 Ghafla vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula na kupata nguvu.
19 Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi.
20 Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
21 Na wote waliosikia walishangaa na kusema, “Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani.”
22 Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri na kuwafanya Wayahudi waliokaa Dameski wachanganyikiwe na kuthibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
23 Baada ya siku nyingi, Wayahudi wakafanya shauri pamoja ili wamuue.
24 Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua.
25 Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu.
26 Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walikuwa wakimuogopa, wasisadiki kuwa yeye ni mwanafunzi.
27 Lakini Barnaba akamchukua na kumpeleka kwa mitume, Na akawaeleza jinsi Sauli alivyomuona Bwana njiani na Bwana alivyosema nae, na jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski.
28 Alikutana nao walipoingia na kutoka Yerusalemu. Akanena kwa ujasiri kwa jina la Bwana Yesu,
29 akihojiana na Wayahudi wa Kiyunani lakini wakijaribu mara kwa mara kumuua.
30 Wakati ndugu walipojua jambo hilo, wakamchukua mpaka Kaisaria, na wampeleke aende Tarso.
31 Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na kutembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi.
32 Kisha ilitokea Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote za mkoa, akawateremkia waumini waishio katika mji wa Lida.
33 Akamuona huko mtu mmoja jina lake Ainea, mtu huyo amekuwa kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.
34 Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo akuponye; Amka na ujitandikia kitanda chako,” Mara akaamka.
35 Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni walipomuona mtu huyo, walimgeukia Bwana.
36 Palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha, ambalo lilitafsiriwa kama “Dorcas” Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya rehema aliyoyafanya kwa maskini.
37 Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza.
38 Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, “Njoo kwetu bila kuchelewa”.
39 Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha koti na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati akiwa pamoja nao.
Matendo ya Mitume 9 in Biblia ya Kiswahili