7 na huko waliihubiri injili.
8 Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, hajawahi kutembea.
9 Mtu huyu alimsikia Paulo akiongea. Paulo alimkazia macho na akaona kwamba alikuwa na imani ya kuponywa.
10 Hivyo alisema kwake kwa sauti ya juu, “Simama kwa miguu yako.” Na yule mtu aliruka juu na kuanza kutembea.
11 Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, “miungu imetushukia kwa namna ya binadamu.”
12 Walimwita Barnaba “Zeu,” na Paulo “Herme” kwa sababu alikuwa msemaji mkuu.
13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka.
14 Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka walikwenda nje kwenye umati, wakilia
15 na kusema, “Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye hisia kama za kwenu. Tunawaletea habari njema, kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo.
16 Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe.
17 Lakini bado, hakuondoka pasipo shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha”
18 Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka.
19 Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa.