Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 14:2-8 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 14:2-8 in Biblia Takatifu

2 Lakini Wayahudi wengine waliokataa kuwa waumini walichochea na kutia chuki katika mioyo ya watu wa mataifa mengine ili wawapinge hao ndugu.
3 Paulo na Barnaba waliendelea kukaa huko kwa muda mrefu. Waliongea kwa uhodari juu ya Bwana, naye Bwana akathibitisha ukweli wa ujumbe walioutoa juu ya neema yake, kwa kuwawezesha kutenda miujiza na maajabu.
4 Watu wa mji huo waligawanyika: wengine waliwaunga mkono Wayahudi, na wengine walikuwa upande wa mitume.
5 Mwishowe, baadhi ya watu wa mataifa mengine na Wayahudi, wakishirikiana na wakuu wao, waliazimu kuwatendea vibaya hao mitume na kuwapiga mawe.
6 Mitume walipogundua jambo hilo, walikimbilia Lustra na Derbe, miji ya Lukaonia, na katika sehemu za jirani,
7 wakawa wanahubiri Habari Njema huko.
8 Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa amelemaa miguu tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
Matendo 14 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 14:2-8 in Biblia ya Kiswahili

2 Lakini wayahudi wasiotii waliwachochea akili wamataifa na kuwafanya kuwa wabaya dhidi ya ndugu.
3 Kwa hiyo walikaa huko kwa muda mrefu, wakiongea kwa ujasiri kwa nguvu ya Bwana, huku akitoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake. Alifanya hivi kwa kutoa ishara na majaabu vifanywe kwa mikono ya Paulo na Barnaba.
4 Lakini eneo kubwa la mji liligawanyika: baadhi ya watu walikuwa pamoja na Wayahudi, na baadhi pamoja na mitume.
5 Wakati wamataifa na Wayahudi walipojaribu kuwashawishi viongozi wao kuwatendea vibaya na kuwaponda mawe Paulo na Barnaba,
6 wakalitambua hilo na kukimbilia katika miji ya Likaonia, Listra na Derbe, na maeneo yanayozunguka pale,
7 na huko waliihubiri injili.
8 Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, hajawahi kutembea.
Matendo ya Mitume 14 in Biblia ya Kiswahili