Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 14:10-28 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 14:10-28 in Biblia Takatifu

10 akasema kwa sauti kubwa, “Simama wima kwa miguu yako!” Huyo mtu aliyelemaa akainuka ghafla, akaanza kutembea.
11 Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, ulianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”
12 Barnaba akaitwa Zeu, na Paulo, kwa vile yeye ndiye aliyekuwa anaongea, akaitwa Herme.
13 Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, na pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume.
14 Barnaba na Paulo walipopata habari hiyo waliyararua mavazi yao na kukimbilia katika lile kundi la watu wakisema kwa sauti kubwa:
15 “Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama ninyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo.
16 Zamani Mungu aliruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda.
17 Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
18 Ingawa walisema hivyo haikuwa rahisi kuwazuia wale watu wasiwatambikie.
19 Lakini Wayahudi kadhaa walikuja kutoka Antiokia na Ikonio, wakawafanya watu wajiunge nao, wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji wakidhani amekwisha kufa.
20 Lakini waumini walipokusanyika na kumzunguka, aliamka akarudi mjini. Kesho yake, yeye pamoja na Barnaba walikwenda Derbe.
21 Baada ya Paulo na Barnabas kuhubiri Habari Njema huko Derbe na kupata wafuasi wengi, walifunga safari kwenda Antiokia kwa kupitia Lustra na Ikonio.
22 Waliwaimarisha waumini wa miji hiyo na kuwatia moyo wabaki imara katika imani. Wakawaambia, “Ni lazima sisi sote tupitie katika taabu nyingi ili tuingie katika ufalme wa Mungu.”
23 Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada ya kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
24 Baada ya kupitia katika nchi ya Pisidia, walifika Pamfulia.
25 Baada ya kuhubiri ule ujumbe huko Perga, walikwenda Atalia.
26 Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.
27 Walipofika huko Antiokia walifanya mkutano wa kanisa la mahali hapo, wakawapa taarifa juu ya mambo Mungu aliyofanya pamoja nao, na jinsi alivyowafungulia mlango watu wa mataifa mengine mlango wa kuingia katika imani.
28 Wakakaa pamoja na wale waumini kwa muda mrefu.
Matendo 14 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 14:10-28 in Biblia ya Kiswahili

10 Hivyo alisema kwake kwa sauti ya juu, “Simama kwa miguu yako.” Na yule mtu aliruka juu na kuanza kutembea.
11 Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, “miungu imetushukia kwa namna ya binadamu.”
12 Walimwita Barnaba “Zeu,” na Paulo “Herme” kwa sababu alikuwa msemaji mkuu.
13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka.
14 Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka walikwenda nje kwenye umati, wakilia
15 na kusema, “Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye hisia kama za kwenu. Tunawaletea habari njema, kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo.
16 Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe.
17 Lakini bado, hakuondoka pasipo shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha”
18 Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka.
19 Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa.
20 Hata hivyo wanafunzi walikuwa wamesimama karibu naye, aliamka, wakaingia mjini. Siku ya pili, aliende Derbe na Barnaba.
21 Baada ya kufundisha injili katika mji ule na kuwafanya wanafunzi wengi, walirudi Listra, hadi Ikoniamu, na hadi Antiokia.
22 Waliendelea kuimarisha nafsi za wanafunzi na kutiwa moyo kuendelea katika imani, akasema, “Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu kwa kupitia mateso mengi.”
23 Walipo wateua kwa ajili yao wazee wa kila kusanyiko la waaminio, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini.
24 Kisha walipita katika Pisidia, walifika Pamfilia.
25 Wakati walipoongea maneno katika Perga, waliteremka kwenda Atalia.
26 Kutoka huko walipanda meli hadi Antiokia ambako walikuwa wamejitoa kwa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameikamilisha.
27 Walipofika huko Antiokia, na kulikusanya kusanyiko la pamoja, wakatoa taarifa ya mambo ambayo Mungu amefanya kwao, na jinsi alivyowafungulia mlango wa imani kwa watu wa Mataifa.
28 Walikaa kwa muda mrefu na wanafunzi.
Matendo ya Mitume 14 in Biblia ya Kiswahili