Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 13:1-8 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 13:1-8 in Biblia Takatifu

1 Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.
2 Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”
3 Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono, wakawaacha waende zao.
4 Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
5 Walipofika Salami walihubiri neno la Mungu katika masunagogi ya Kiyahudi. Yohane (Marko) alikuwa msaidizi wao.
6 Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Baryesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
7 Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
8 Lakini huyo mchawi Elima (kama alivyokuwa anaitwa kwa Kigiriki), alijaribu kuwapinga ili kumzuia huyo mkuu wa kisiwa asije akaigeukia imani ya Kikristo.
Matendo 13 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 13:1-8 in Biblia ya Kiswahili

1 Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaeni (ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli.
2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, “Niteengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia.”
3 Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende.
4 Kwa hiyo Barnabas na Sauli walimtii Roho Mtakatifu na walitelemka kuelekea Seleukia; Kutoka huko walisafiri baharini kuelekea kisiwa cha Kipro.
5 Walipokuwa katika mji wa Salami, walilitangaza neno la Mungu katika Masinagogi ya Wayahudi. Pia walikuwa pamoja na Yohana Marko kama msaidizi wao.
6 Walipokwenda katika kisiwa chote mpaka Pafo, walikuta mtu fulani mchawi, Myahudi nabii wa uongo, ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu.
7 Mchawi huyu alishirikiana na Liwali Sergio Paulus, aliyekuwa mtu mwenye akili. Mtu huyu aliwaalika Barnaba na Sauli, kwa sababu alihitaji kusikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima “yule mchawi” (hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa) aliwapinga; alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani.
Matendo ya Mitume 13 in Biblia ya Kiswahili