Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Matendo - Matendo 13

Matendo 13:1-8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.
2Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”
3Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono, wakawaacha waende zao.
4Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
5Walipofika Salami walihubiri neno la Mungu katika masunagogi ya Kiyahudi. Yohane (Marko) alikuwa msaidizi wao.
6Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Baryesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
7Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
8Lakini huyo mchawi Elima (kama alivyokuwa anaitwa kwa Kigiriki), alijaribu kuwapinga ili kumzuia huyo mkuu wa kisiwa asije akaigeukia imani ya Kikristo.

Read Matendo 13Matendo 13
Compare Matendo 13:1-8Matendo 13:1-8