Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 11:4-13 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 11:4-13 in Biblia Takatifu

4 Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juu ya yale yaliyotendeka tangu mwanzo:
5 “Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa likishushwa chini kutoka mbinguni likiwa limeshikwa pembe zake nne, likawekwa kando yangu.
6 Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
7 Kisha nikasikia sauti ikiniambia: Petro amka, chinja, ule.
8 Lakini mimi nikasema: La, Bwana; maana chochote kilicho najisi au kichafu hakijapata kamwe kuingia kinywani mwangu.
9 Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.
10 Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni.
11 Ghafla, watu watatu waliokuwa wametumwa kwangu kutoka Kaisarea waliwasili kwenye nyumba niliyokuwa nakaa.
12 Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa Kornelio.
13 Yeye alitueleza jinsi alivyokuwa amemwona malaika amesimama nyumbani mwake na kumwambia: Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.
Matendo 11 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 11:4-13 in Biblia ya Kiswahili

4 Lakini Petro alianza kueleza tukio kwa kina; akisema,
5 “Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu.
6 Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa polini na wanyama watambaao na ndege wa angani.
7 Kisha nikasikia sauti ikisema nami, “Amka, Petro, chinja naj ule!”
8 Nikasema, “Siyo hivyo, Bwana, mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu”
9 Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi,
10 Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.
11 Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu.
12 Roho akaniambia kwenda nao, na nisitofautiane nao. Hawa wanaume sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu mmoja.
13 Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, “Nitume Yafa nikamlete simoni ambaye jina lake lingine ni Petro.
Matendo ya Mitume 11 in Biblia ya Kiswahili