Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 9

Mambo ya Walawi 9:5-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Kwa hiyo wakaleta kwenye hema la kukutania vyote ambavyo Musa aliagiza, nalo kusanyiko lote la Israeli likakaribia na kusimama mbele za Yahweh.
6Kisha Musa akasema, “Hivi ndivyo Yahweh amewaamru nyinyi mfanye, ili kwamba utukufu wake uweze kuonekana kwenu.
7“Musa akamwambia Aroni, “Njoo karibu na Madhabahu na uteo sadaka yako ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu ili kufanya upatanisho kwa ajili yao kama vile ambavyo Yahweh amekwishaamru.”
8Kwa hiyo Aroni akaikaribia madhabahu na akamchinja yule ndama kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ambayo ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe.
9Nao wana wa Aroni wakamletea hiyo damu, naye akakichofya kidole chake kwenye damu na kuiweka kwenye pembe za madhabahu, kisha akaimwaga damu chini ya kitako cha madhabahu.
10Hata hivyo, aliyateketeza hayo mafuta, figo, na mafuta yanafunika ini juu ya madhabahu kuwa sadaka ya dhambi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
11Na akaiteketeza hiyo nyama pamoja na ngozi nje ya kambi
12Aroni akaichinja sadaka ya kuteketezwa, nao wanawe wakampa hiyo damu, ambayo aliinyunza pande zote za madhabahu.
13Kisha wakampa ile sadaka ya kuteketezwa, kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.
14Akaziosha sehemu za ndani pamoja na miguu na kuziteketeza juu ya dhabihu ya kuteketezwa juu ya Madhabahu.
15Aroni akaleta dhabihu ya watu— mbuzi, kisha akamtoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi yao naye akamchinja, akaitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi, kama alivyofanya kwa yule mbuzi wa kwanza.
16Akaileta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama Yahweh alivyokuwa ameamru.
17Akaileta sadaka ya nafaka; akakijaza kiganja chake nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa.
18Pia akamchinja fahali na yule kondoo dume, dhabihu kwa ajili ya sadaka ya amani, ambayo ilikuwa kwa ajili ya watu. Nao wana wa Aronni wakampa damu, ambayo aliinyunyiza kila upande wa mdhabahu.
19Hata hivyo, waliyakata mafuta ya fahali na ya yule kondoo dume, mafuta ya kwenye mkia, mafuta yafunikayo sehemu za ndani, figo, na yale mafuta yaliyofunika mapafu.
20Wakazichukua hizi sehemu zilizokatwa wakaziweka juu ya vidari, na kisha Aroni akateketeza mafuta juu ya madhabahu.
21Naye Aroni akavitikisa vidari na paja la kulia kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh, kama vile Musa alivyokuwa ameamru,
22Kisha Aroni akainua juu mikono yake mbele ya watu na kuwabariki, kisha akashuka chini kutoka mahali alipokuwa akitoa hiyo sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani.
23Musa na Aroni wakaingia ndani ya hema la kukutania, kisha wakatoka nje tena na kuwabariki watu, na utukufu wa Yahweh ukaonekana kwa watu wote.

Read Mambo ya Walawi 9Mambo ya Walawi 9
Compare Mambo ya Walawi 9:5-23Mambo ya Walawi 9:5-23