16Yeye anayelikufuru jina la Yahweh kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahweh, ni lazima auawe.
17Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auewa.
18Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.
19Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:
20Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.
21Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.