Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 20

Mambo ya Walawi 20:20-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao.
21Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote amabayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao.
22Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi.
23Msienende katika desturi za mataifa ambayo nitayafukuza mbele yenu, ni kwa sababu wamefanya mambo haya yote, nami mimewachukia wao.
24Nami nikawaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao, nitaitoa kwenu ili muimiliki, nchi itiririkayo amaziwa na asali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine.
25Ni lazima pia mtofautishe kati ya wanya najisi na wale walio safi, na kati ya ndege walio najisi na walio safi. Msijichafue wenyewe kwa wanyama au ndege au kiumbe kitambaacho juu ya nchi kilicho najisi, ambacho nimekitenga kuwa najisi.
26Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi, Yahweh, ni mtakakatifu, nami nimewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine, kwa kuwa nyinyi ni wangu.
27Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.

Read Mambo ya Walawi 20Mambo ya Walawi 20
Compare Mambo ya Walawi 20:20-27Mambo ya Walawi 20:20-27