Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 15

Mambo ya Walawi 15:19-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
20Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
21Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
22Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
23Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
24Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.
25Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.
26Kila kitanda anachokilalia wakati wote wa kutokwa damu itakuwa kwake sawa tu kama kitanda anacholalia wakati wa hedhi, na kila kitu ambacho anakalia kitakuwa najisi, kama tu unajisi wa hedhi yake.

Read Mambo ya Walawi 15Mambo ya Walawi 15
Compare Mambo ya Walawi 15:19-26Mambo ya Walawi 15:19-26