Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mambo ya Walawi 15:19-26 in Swahili (individual language)

Help us?

Mambo ya Walawi 15:19-26 in Biblia ya Kiswahili

19 Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
20 Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
21 Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
22 Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
23 Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
24 Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.
25 Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.
26 Kila kitanda anachokilalia wakati wote wa kutokwa damu itakuwa kwake sawa tu kama kitanda anacholalia wakati wa hedhi, na kila kitu ambacho anakalia kitakuwa najisi, kama tu unajisi wa hedhi yake.
Mambo ya Walawi 15 in Biblia ya Kiswahili