Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 11

Mambo ya Walawi 11:9-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala ni wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni.
10Lakini viumbe wote hai wasio na mapezi na magamba waliomo baharini au mitoni, pamoja na wale waendao majini na viumbe hai waliomo majini —watakuwa chukizo kwenu.
11Kwa kuwa watakuwa chukizo, msile nyama yao, pia mizoga yao sharti itakuwa chukizo.
12Chochote kisichokuwa na mapezi au magamba kilichomo majini ni lazima kiwe chukizo kwenu.
13Nao ndege mtakaowachukia na msiopaswa kuwala ni hawa wafuatao: tai, furukombe, kipungu,
14mwewe mwekundu, aina yoyote ya kipanga,
15kila aina ya kunguru,
16kiruka-njia, kipasuasanda, Shakwe, na aina yoyote ya mwewe.
17Ni lazima pia bundi mdogo na bundi mkubwa muwaone kuwa chukizo, mnandi,
18bundi mweupe na mwari,

Read Mambo ya Walawi 11Mambo ya Walawi 11
Compare Mambo ya Walawi 11:9-18Mambo ya Walawi 11:9-18