Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 20

Luka 20:1-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika,
2wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?”
3Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali:
4mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”
5Lakini wao wakajadiliana hivi: “Tukisema yalitoka mbinguni, yeye atatuuliza: Mbona hamkumsadiki?
6Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii.”
7Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.”
8Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.”
9Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
10Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.
11Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.
12Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.
13Yule mwenye shamba akafikiri: Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.
14Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: Huyu ndiye mrithi. Basi, tumwue ili urithi wake uwe wetu.

Read Luka 20Luka 20
Compare Luka 20:1-14Luka 20:1-14