Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 1:8-16 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 1:8-16 in Biblia Takatifu

8 Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu,
9 Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani.
10 Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani.
11 Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.
12 Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
13 Lakini malaika akamwambia, “Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
14 Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake.
15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
16 Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao.
Luka 1 in Biblia Takatifu

Luka 1:8-16 in Biblia ya Kiswahili

8 Sasa ilitokea kwamba Zakaria alikuwa katika uwepo wa Mungu, akiendelea na wajibu wa kikuhani katika utaratibu wa zamu yake.
9 Kulingana na desturi ya kuchagua ni kuhani yupi atakayehudumu, alikuwa amechaguliwa kwa kura kuingia katika hekalu la Bwana na hivyo angefukiza uvumba.
10 Kundi lote la watu lilikuwa likiomba nje wakati wa kufukizwa kwa ufumba.
11 Sasa malaika wa Bwana alimtokea na kasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia.
12 Zakaria alitishika alipomuona; hofu ikamwangukia.
13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope Zakaria, kwasababu maombi yako yamesikika. Mke wako Elizabeth atakuzalia mwana. Jina lake utamwita Yohana.
14 Utakuwa na furaha na uchangamfu, na wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.
15 Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
16 Na watu wengi wa Israel watageuzwa kwa Bwana Mungu wao.
Luka 1 in Biblia ya Kiswahili