48 Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
49 Kwa maana yeye aliyemweza amefanya mambo makubwa kwangu, na jina lake ni takatifu.
50 Rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mheshimu yeye.
51 Ameonesha nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
52 Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
53 Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54 Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55 (kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”
56 Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
57 Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.
58 Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.
59 Sasa ilitokea siku ya nane kwamnba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zekaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake,
60 Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.”
61 Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.”
62 Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.
63 Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili.
64 Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.
65 Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.
66 Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, “Mtoto huyu kuwa wa namna gani?” Kwasababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
67 Baba yake Zekaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
68 “Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
69 Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
70 kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
71 Atatuoka kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72 Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
73 kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
74 Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu.
75 katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.
76 Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
77 kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.