Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 10

Luka 10:11-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11'Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.'
12Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahamilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo.
13Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, Wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu.
14Lakini itakuwa usitahamilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu.
15Wewe Kapernaumu, Unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu
16Atakaye wasikiliza ninyi anisikiliza mimi, na yeyote atakaye wakataa anikataa mimi, na yeyote anikataaye mimi anmtakaa aliyenituma”
17Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”
18Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.
19Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.
20Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.”
21Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”

Read Luka 10Luka 10
Compare Luka 10:11-21Luka 10:11-21