Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 7:5-10 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 7:5-10 in Biblia ya Kiswahili

5 Ikiwa sisemi ukweli basi umruhusu adui yangu kuyaingilia maisha yangu na kuyaharibu; na umuache aukanyage mwili wangu ulio hai kwenye aridhi na kuuacha umelala kwa aibu mavumbini. Selah
6 Inuka, Yahweh, katika hasira yako; simama kinyume na hasira kali ya adui zangu; amka kwa ajili yangu na ubebe amri zako ambazo wewe umeamuru kwa ajili yao.
7 Mataifa yote yamekuzunguka; uwatawale kutoka mbinguni.
8 Yahweh, uwahukumu mataifa; uwaonyeshe kuwa sina hatia, Yahweh, kwa sababu mimi ni mwenye haki na sina hatia, Ewe uliye juu.
9 Matendo ya waovu na yafike mwisho, bali uanzishe watu wenye haki, Mungu mwenye haki, wewe ambaye unapima mioyo na fahamu.
10 Ngao yangu inatoka kwa Mungu, yule anaye okoa moyo wa mwenye haki.
Zaburi 7 in Biblia ya Kiswahili