Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 72:2-17 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 72:2-17 in Biblia ya Kiswahili

2 Naye awaamue watu wako kwa haki na maskini wako kwa haki sawa.
3 Milima iwazalie watu amani; vilima navyo vizae haki.
4 Naye awahukumu watu maskini; awaokoe watoto wa wahitaji na kuwavunja vipande vipande wenye kuwatesa.
5 Na wakuheshimu wewe wakati wa jua, na kwa kipindi cha kudumu kwa mwezi katika vizazi vyote.
6 Naye apate kuja kama mvua juu ya nyasi zilizokatwa, kama manyuyu yanyunyizayo nchi.
7 Mwenye haki na astawi kwa wakati wake, na amani iwepo kwa wingi mpaka mwezi utakapotoweka.
8 Na awe na mamlaka toka bahari na bahari, na kutoka Mto hadi miisho ya dunia.
9 Na wote waishio jangwani wainame mbele zake; adui zake na walambe mavumbi.
10 Wafalme wa Tashishi na visiwa walete kodi; wafalme wa Sheba na Seba watoe zawadi.
11 Hakika wafalme wote wamwinamie yeye; mataifa yote yamtumikie yeye.
12 Kwa kuwa yeye humsaidia mhitaji na maskini asiye na msaidizi.
13 Yeye huwahurumia maskini na wahitaji, na huokoa maisha ya wahitaji.
14 Huyaokoa maisha yao dhidi ya mateso na vurugu, na damu yao ni ya thamani machoni pake.
15 Naye apate kuishi! Na dhahabu za Sheba apewe yeye. Watu wamuombee yeye siku zote; Mungu ambariki daima.
16 Kuwepo na nafaka nyingi katika ardhi; juu ya milima kuwe na mawimbi ya mimea. Matunda yake yawe kama Lebanoni; watu wasitawi katika miji kama nyansi za kondeni.
17 Jina lake lidumu milele; jina lake ilindelee kama vile jua ling'aavyo; watu wabarikiwe katika yeye; mataifa yote wamwite mbarikiwa.
Zaburi 72 in Biblia ya Kiswahili