Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 72

Zaburi 72:2-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Naye awaamue watu wako kwa haki na maskini wako kwa haki sawa.
3Milima iwazalie watu amani; vilima navyo vizae haki.
4Naye awahukumu watu maskini; awaokoe watoto wa wahitaji na kuwavunja vipande vipande wenye kuwatesa.
5Na wakuheshimu wewe wakati wa jua, na kwa kipindi cha kudumu kwa mwezi katika vizazi vyote.
6Naye apate kuja kama mvua juu ya nyasi zilizokatwa, kama manyuyu yanyunyizayo nchi.
7Mwenye haki na astawi kwa wakati wake, na amani iwepo kwa wingi mpaka mwezi utakapotoweka.
8Na awe na mamlaka toka bahari na bahari, na kutoka Mto hadi miisho ya dunia.
9Na wote waishio jangwani wainame mbele zake; adui zake na walambe mavumbi.
10Wafalme wa Tashishi na visiwa walete kodi; wafalme wa Sheba na Seba watoe zawadi.
11Hakika wafalme wote wamwinamie yeye; mataifa yote yamtumikie yeye.
12Kwa kuwa yeye humsaidia mhitaji na maskini asiye na msaidizi.
13Yeye huwahurumia maskini na wahitaji, na huokoa maisha ya wahitaji.
14Huyaokoa maisha yao dhidi ya mateso na vurugu, na damu yao ni ya thamani machoni pake.
15Naye apate kuishi! Na dhahabu za Sheba apewe yeye. Watu wamuombee yeye siku zote; Mungu ambariki daima.
16Kuwepo na nafaka nyingi katika ardhi; juu ya milima kuwe na mawimbi ya mimea. Matunda yake yawe kama Lebanoni; watu wasitawi katika miji kama nyansi za kondeni.
17Jina lake lidumu milele; jina lake ilindelee kama vile jua ling'aavyo; watu wabarikiwe katika yeye; mataifa yote wamwite mbarikiwa.

Read Zaburi 72Zaburi 72
Compare Zaburi 72:2-17Zaburi 72:2-17