Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 37:16-30 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 37:16-30 in Biblia ya Kiswahili

16 Ni bora kuwa mwenye haki maskini kuliko tajiri mwenye mali nyingi.
17 Kwa maana mikono ya watu waovu itavunjika, bali Yahwe huwasaidia watu wenye haki.
18 Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha.
20 Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
21 Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
22 Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
23 Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
24 Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake.
25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
26 Wakati wote yeye ni mkarimu na hukopesha, nao watoto wake hufanyika baraka.
27 Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele.
28 Kwa maana Yahwe hupenda haki naye hawaachi wafuasi waaminifu. Wao hutunzwa milele, lakini uzao wa waovu utafutiliwa mabli.
29 Wenye haki watairithi nchi na kuaa huko milele.
30 Mdomo wa mwenye haki huongea hekima na huongeza haki.
Zaburi 37 in Biblia ya Kiswahili