15 Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
16 Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
17 Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
18 Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
19 Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!
20 Uiokoe roho yangu na upanga, maisha yangu mwenyewe na makucha ya mbwa mwitu.
21 Uniokoe na mdomo wa simba; uniokoe na mapembe ya ng'ombe wa porini.
22 Nami nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kusanyiko la watu nitakusifu wewe.