17 kwa kuwa ni Yahweh Mungu wetu ambaye alitutoa sisi na baba zetu kutoka katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, na ambaye alifanya hizo ishara kubwa mbele yetu, na ambaye alituhifadhi sisi katika njia zote ambazo sisi tuliziendea, na miongoni mwa mataifa yote ambayo tulipita kati kati yake,
18 Na Yahweh aliwaondoa mbele yetu watu wote, na Waamori walioishi katika nchi hii. Hivyo, tutamwabudu Yahweh pia, kwa kuwa ni Mungu wetu”
19 Lakini Yoshua akawaambia watu, “Hamwezi kumtumikia Yahweh, kwa kuwa ni Mungu mtakatifu; ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa na dhambi zenu.
20 Kama mtamwacha Yahweh na kuabudu miungu ya kigeni, basi atageuka na kuwaharibu. Atawaangamizeni baada ya kuwa amewatendea mema.”
21 Lakini watu walimwambia Yoshua, “Hapana, tutamwabudu Yahweh.”
22 Kisha Yoshua akawaambia watu, “Ninyi ni mashahidi dhidi yenu wenyewe kuwa mmemchagua Yahweh ninyi wenyewe, ili mmwabudu yeye.” Watu walijibu, “Sisi ni mashahidi.”
23 “Sasa wekeni mbali miungu ya kigeni iliyoko kwenu, na geuzeni moyo wenu umwelekee Yahweh, Mungu wa Israeli.”