Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 15:17-60 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 15:17-60 in Biblia ya Kiswahili

17 Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake na Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.
18 Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, “Unataka nini?”
19 Akisa akamjibu, “Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negevu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji.” Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.
20 Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na koo zao.
21 Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,
22 Kina, Dimona, Adada,
23 Kadeshi, Hazor, Ithinani,
24 Zifu, Telemu, Bealothi.
25 Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),
26 Amamu, shema, Molada,
27 Hazari Gada, Heshimoni, Bethi Peleti,
28 Hazari Shuali, Beerisheba, Biziothia.
29 Baala, Limu, Ezemu,
30 Eltoladi, Kesili, Horma,
31 Ziklagi, Madimana, Sansana,
32 Lebaothi, Shilihimu, Aini, na Rimoni. Miji hii ilikuwa ishirini na tisa kwa ujumla, kujumlisha na vijiji vyake.
33 Katika nchi iliyo chini ya mlima upande wa magharibi, kulikuwa na miji ya Eshtaoli, Zora, Ashina,
34 Zanaoa, Eni Ganimu, Tapua, Enamu,
35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
36 Shaaraimu, Adithaimu, na Gedera (ambayo ndio Gederothaimu). Hesabu ya miji hii ilikuwa ni kumi na nne, pamoja na vijiji vyao.
37 Zena, Hadasha, Migidagadi,
38 Dileani, Mizipa, Yokitheeli,
39 Lakishi, Bozikathi, Egloni.
40 Kaboni, Lahmamu, Kitilishi,
41 Gederothi, Bethi Dagoni, Naama, Makeda. Hesabu ya miji hii ilikuwa kumi na sita, kujumlisha na vijiji vyao.
42 Libna, Etheri, Ashani,
43 Ifuta, Ashina, Nezibu,
44 Keila, Akizibu, na Maresha. Hii ilikuwa ni miji tisa, kujumlisha na vijiji vyao.
45 Ekroni, pamoja na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka;
46 kutoka Ekroni kuelekea Bahari Kuu, makazi yote ambayo yalikuwa karibu na Ashidodi, pamoja na vijiji vyake.
47 Ashidodi, na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; Gaza na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; hata kufika kijito cha Misri, na kuelekea Bahari Kuu pamoja na ukanda wake wa pwani.
48 Katika nchi ya milima, kuna miji ya Shamiri, Yatiri, Soko,
49 Dana, Kiriathi Sana (ambayo ndio Debiri),
50 Anabu, Eshitemo, Animu,
51 Gosheni, Holoni, na Gilo. Hii ilikuwa ni miji kumi na moja, kujumuisha na vijiji vyake.
52 Arabu, Duma, Ehani,
53 Yanimu, Bethi Tapua, Afeka,
54 Humta, Kiriathi Arba (ambayo ndio Hebroni), na Ziori. Hii ilikuwa miji tisa, pamoja na vijiji vyake.
55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
57 Kaini, Gibea, na Timna. Hii ilikuwa ni miji kumi, kujumuisha na vijiji vyake.
58 Halhuli, Bethi Zuri, Gedori,
59 Maarathi, Bethi Anothi, na Elitekoni. Hii ilikuwa miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60 Kiriathi Baali (ambayo ndio Kiriathi Yearimu), na Raba. Hii ilikuwa ni miji miwili, pamoja na vijiji vyake.
Yoshua 15 in Biblia ya Kiswahili