Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 15:15-26 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 15:15-26 in Biblia ya Kiswahili

15 Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
16 Kalebu akasema, “Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.
17 Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake na Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.
18 Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, “Unataka nini?”
19 Akisa akamjibu, “Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negevu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji.” Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.
20 Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na koo zao.
21 Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,
22 Kina, Dimona, Adada,
23 Kadeshi, Hazor, Ithinani,
24 Zifu, Telemu, Bealothi.
25 Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),
26 Amamu, shema, Molada,
Yoshua 15 in Biblia ya Kiswahili